Zebramotief met 'Maartense Aid Fund' Mikumi Health Centre , Tanzania

Kelters sasa tulia.



1.
Ni siku yenye furaha, mgeni kutufikia,
Richard mwenye furaha, Mikumi kwetu tulia,
Wafanyakazi twahaha, sifa zako ndizo mia.
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.

2.
Tarifa tulizipata, kama wewe unafika,
Hatukupenda kunata, ila tumefadhaika,
Na sasa twajitafuta, ili wote jumuika,
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.

3.
Imani kwako tunayo, misada mingi kuleta,
Leo twapiga mayoyo, hakuna kwetu matata
Twakupongeza kwa moyo, mfadhiri tumepata,
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.

4.
Ni moyo wa ujasiri, Mzungu kweli mzungu,
Richard tumekubali, kweli wewe ni mzungu,
Kutoa umekubali, na pesa zote mafungu,
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.

5.
Maabra wafurahi, vifaa vingi kupata,
Maternity ni kuwahi, vifaa vingi kupata,
Kituo umekiwahi, umekipaka kiroho,
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.

6.
Wafanyakazxi twasema, saidia 'paka mwisho,
Usijeanza simama, tukapatwa na kihoho,
Afya kwako ni uzima, twakuombea kiroho,
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.

7.
Asali tulioamba, uliyeleta ni wewe,
Richard kweli ni mwamba, Mungu awe pamwe nawe,
Usituache wembamba, ni bora tuwe na wewe,
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.

8.
Misada uiongeze, siku zote maishani,
Kidogo ndio tuanze, Richard hapa nyumbani,
Na sisi tukaitunze, misadayo kwa makini,
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.

9.
Tunaomba zingatia, yote tuliyoeleza,
Na moyo uje tutia, na kituo kwendeleza,
Daima twakutakia, unfanye unaloweza,
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.

10.
Mwisho baraka twatoa, mpendwa wetu husika,
Maisha twakutakia, mema yenye kusifika,
Furaha twakutakia, tuzidi kunufaika,
Mgeni wetu karibu, hapa kwetu umefika.
Giro rekening: 9237166   
t.n.v. Maartense Aid Fund  
te Lelystad  
Maartense Aid Fund